ads

adds

AZAM FC WAIFANYIA UMAFIA YANGA MCHANA KWEUPE


Klabu ya Azam FC imemrudisha nyumbani mchezaji wake wa zamani Awesu Awesu  aliyekuwa akiichezea Kagera Sugar msimu wa 2019/20. Awesu  alianzia maisha yake ya soka Azam Academy mwaka 2015 na baadaye alijiunga na Madini fc ya Arusha kisha Mwadui ,Singida United na baadaye Kagera Sugar .

Mchezaji huyo alikuwa kwenye hesabu za Yanga tangu dirisha dogo na alitakiwa kusajiliwa kwa msimu wa 2020/21 lakini Azam FC walimuwahi kimya kimya na kumsajilli hii leo tarehe 30 Julai . Kupitia mitandao yake ya kijamii Azam FC waliandika
"Azam FC tunayo furaha kubwa kuwataarifu kuwa tumekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu, kwa mkataba wa miaka miwili.Awesu anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam FC kwenye dirisha kubwa la usajili kwa ajili ya msimu ujao, ukiwa ni usajili huru baada ya kumaliza mkataba wake Kagera Sugar.
Kiungo huyo ambaye aliwahi kulelewa kwenye kituo cha Azam Academy kwa miaka miwili 2014-2015, amesaini mkataba huo leo Alhamisi jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Nyota huyo amekuwa na kiwango kizuri kwa misimu miwili mfululizo akiwa na Singida United na msimu huu Kagera Sugar, katika mashindano yote msimu huu akiwa amefunga jumla ya mabao saba.
Imemchukua safari ya miaka mitano kwa Awesu kurejea tena Azam FC, baada ya kuondoka Azam Academy mwaka 2015, akijiunga na Madini ya Arusha, kabla ya kutua Mwadui kisha Singida United na msimu uliopita Kagera Sugar.

Awesu akisaini mkataba



Post a Comment

0 Comments