Msemaji na afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara amesema viongozi wa klabu ya Yanga wanatakiwa kufanya maamuzi magumu hasa kwa wachezaji watukutu kama Morrison.Manara amewakumbusha viongozi wa Yanga kuhusu tabia za utovu wa nidhamu wa Morrison ikiwemo kutoroka kambini,kuwashikia viongozi kisu na hata kutoka uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko. Manara amenukuliwa akisema
"Juzi juzi tu hapa Yanga walisema wametushitaki TFF kwa kosa la kumrubuni Morrison, pia Morrison huyohuyo akawapeleka TFF akidai hajasaini mkataba na Young Africans Sports club"
"Pia Morrison huyohuyo akawatolea kisu kambini kwao. Pia wao wenyewe wakatuonesha kupitia vyombo vya habari kuwa Morrison kawazimia simu, kama haitoshi Morrison huyohuyo akafanya exclusive interview na kuwasema viongozi wa Yanga.... Mmemlea yote hayo mnategemea nini ?! Hilo la kwanza"
Manara aliongeza kwa kusema klabu ya Simba imekuwa imara sana kiasi cha kwamba wapinzani wa klabu hiyo wamekubali uwezo wao na kuanza kulaumu wachezaji wao
"Lapili leo asubuhi nimemsikia rafiki yangu Nugaz akisema wamefungwa kwa sababu ya makandokando,, kwamba wachezaji wa Yanga wamewasaliti (Wamenunuliwa) ...Unasema hivyo hadharani unategemea wachezaji watakuheshimu ?! Wachezaji waliojitoa, wakawapa matokeo march (8) leo unawaita wasaliti!!"
0 Comments