ads

adds

YANGA WAREJEA NAFASI YA PILI KIBABE


Yanga SC wametokea nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Ndanda SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Ushindi huo unairejesha Yanga SC nafasi ya pili, ikifikisha pointi 60 katika mchezo wa 32, sasa inazidiwa pointi 18 na mabingwa watetezi, SImba SC ambao wana mechi moja mkononi. 
 
Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Raphael Ikambi wa Morogoro aliyesaidiwa na Sunday Komba wa Kilimanjaro na Credo Mbuya wa Mbeya, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wake, Deus David Kaseke dakika ya tano tu akimalizia pasi ya mshambuliaji Ditram Adrian Nchimbi.


Lakini Ndanda SC wakatoka nyuma kwa mabao mawili ya Abdul Hamisi dakika ya 10 na 15 mara zote akimalizia kazi nzuri ya mchezaji mwenzake Omary Mponda na kuongoza kwa 2-1.
Mchezaji wa zamani wa Mbeya City, Deus Kaseke akaisawazishia Yanga dakika ya 45 akimalizia kazi nzuri ya beki wa kulia, Juma Abdul Mnyamani.Mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa akatokea benchi kipindi cha pili na kuifungia Yanga SC bao la ushindi dakika ya 72 akimalizia kazi nzuri ya Juma Abdul.


Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Adeyoum Ahmed, Said Juma ‘Makapu’, Kelvin Yondan, Feisal Salum, Haruna Niyonzima/ Patrick Sibomana dk78, Raphael Daudi/ Abdulaziz Makame dk46, David Molinga/ Tariq seif dk78, Ditram Nchimbi/Mrisho Ngassa dk64 na Deus Kaseke.

 
Ndanda SC; Ally Mustapha ‘Barthez’, Swalehe Abdallah, Hemed Khoja, Abdulrazak Mohamed, Paul Maona, Danald Taro, Abdul Hamisi/ Kassim Mdoe dk70, Vitalis Mayanga, Omar Mponda/Athumani Chubi dk85, Omary Ramadhani/Omary Hamisi dk80 na Kiggi Makassy.


Post a Comment

0 Comments