BETI NASI UTAJIRIKE

WACHEZAJI SIMBA HAKUNA KULALA WAWASHANGAZA MASHABIKI MBEYA


Klabu ya Simba iliondoka jana alfajiri kuelekea jijini Mbeya kwa michezo miwili ule wa Mbeya City na Prisons. Mara baada ya kutua tu uwanjani ilielekea kambini na kuanza mazoezi makali kitu kilichowashangaza mashabiki wa soka mkoani humo.

Baadhi ya mashabiki walidhani klabu hiyo itaanza mazoezi siku ya pili ya safari ambayo ni leo lakini walianza mazoezi mara baada tu ya kutua jijini humo. 

Amospoti.com ilipata wasaa wa kuzungumza na mashabiki mbali mbali na mmoja wao alinukuliwa akisema "Hawa akina matola hawataki utani na ubingwa aisee, sisi tulijua timu itapumzika baada ya safari lakini wao wamefikia uwanjani tea kwa mazoezi makali mno. Kweli Simba ya mwaka huu ni baba lao"

Hivi ndivyo wachezaji wa Simba walivyoanza mazoezi makali

Post a Comment

0 Comments