BETI NASI UTAJIRIKE

VIFAHAMU VYANZO VIKUBWA VINNE VINAVYOMFANYA RONALDO KUWA BILIONEAMshambuliaji wa Juventus na taifa la Ureno Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mwanasoka wa kwanza kuwa bilionea duniani. Ronaldo mwenye miaka 35 amekuwa kwenye ubora kwa miaka 12 mfululizo na kumfanya awe analipwa mshahara mkubwa kwa vilabu vya Manchester United ,Real Madrid na sasa Juventus. Je unavifahamu vyanzo vya mapato ya Cristiano Ronaldo? hivi hapa ni vyanzo vyake.

1. Mshahara wake 

Kwa mwaka 2019 Cristiano alipokea mshahara wa dola milioni 85 na kumfanya awe mchezaji wa pili kwa kulipwa mshahara mkubwa baada ya Messi. Akiwa Manchester United,Real Madrid na sasa Juventus amekuwa akilipwa kiasi cha paundi milioni 500 na mkataba wake dhidi ya juventus mpaka mwaka 2022 utamfanya kulipwa mshahara wa paundi milioni 600.

2. Mikataba ya Udhamini 

Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza duniani kwa wingi wa mikataba na makampuni mbalimbali duniani. Ronaldo amesaini mkataba wenye thamani ya dola bilioni 1 na kampuni ya Nike huku pia akiwa balozi wa KFC,Herbalife,Tag Heuer,American Tourister na Egyptian steel.

3. Uwekezaji katika mahotel

Pestana CR7 ni hotel ambazo Cristiano Ronaldo anahisa ndani yake . mshambuliaji huyo wa Juventus anahotel kwenye miji mbalimbali barani ulaya kuanzia Barcelona,Madrid ,Lisbon na kumfanya awe mchezaji mwenye uwekezaji mkubwa kwa upande wa mahoteli ya nyota 4 mpaka 5

4. Uwekezaji katika mavazi

Ronaldo anabrand yake ya mavazi,ifahamikayo kama CR7 inayouza nguo mbalimbali za kiume kuanzia mashati,jeans,tshirt ,viatu na hata pafyumu . kupitia brand hiyo mchezaji huyo amekuwa akijipatia fedha nyingi mno.

Ronaldo amekuwa akijipatia umaarufu ndani na nje ya uwanja ,je unatamani kuona mali anazomiliki baada ya kutajirika ? fuatana nami kupitia makala inayofuata.

Post a Comment

0 Comments