BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI: REKODI ZINAIBEBA MANCHESTER UNITED DHIDI YA TOTTENHAM


Manchester United chini ya Ole Gunnar inahitaji ushindi dhidi ya Tottenham kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza ili iweze kuingia top four na kucheza ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu wa 2020/21 . Swali linakuja je ataweza kuifunga Tottenham ya Jose Mourinho?

Kikosi cha Ushindi kwa Manchester United 
Kikosi cha Manchester United kitaongozwa na De Gea,Wan Bissakha, Maguire,Bailly,Luke shaw,Fred,Bruno Fernandes,Pogba,Martial,Rashford na James .

Hiki ni kikosi chenye uwezo wa kucheza mpira wa kasi kuanzia viungo mpaka washambuliaji.Naamini kama Ole atapanga kikosi hiki basi matokeo yatakuwa uande wake \

Rekodi za Manchester na Tottenham 

Totenham imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Manchester United tangu mwaka 2018 wakishinda mabao 3-0 chini ya kocha Pochetino.Michezo mitano iliyofuta Tottenham hajashinda wala kupata sare dhidi ya Manchester United . 

Tottenham anaingia uwanjani kama Underdog mwenye kiu ya kushinda mchezo huu ili kujisogeza mpaka nafasi ya nne. 

Michezo  mitano  aliyocheza Manchester United kabla ya ligi kusimama alishinda minne na sare moja  huku akiushangaza ulimwengu baada ya kuzifunga Chelsea na Machester City.

Michezo mitano aliyocheza Tottenham kabla ya ligi kusimama alishinda mchezo mmoja sare mbili na vipigo viwili.

Rekodi zinaibeba Manchester United lakini mpira ni dakika 90 tukutane baadaye vibanda umiza


Post a Comment

0 Comments