BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAPILI TAREHE 21-06-2020

Manchester City iko tayari kumuchailia winga wa Ujerumani Leroy sane 24 kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa kandarasi yake iwapo klabu ya Ujerumani ya Bayern Munchen itaongeza thamani yake ya pauni milioni 30.. (Independent)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil anataka kukamilisha kandarasi yake akiichezea Arsenal licha ya kwamba The Gunners inataka kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 , ambaye analipwa kitita cha 350,000 kwa wiki mwisho wa msimu huu kutokana na sababu za kifedha. (ESPN)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard amekana kwamba klabu ya Chelsea itafadhili uhamisho wa mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 21, na beki wa kushoto wa Leicester na England Ben Chilwell, 23, kwa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 29, mwisho wa msimu huu . (Guardian)

Mesut Ozil anataka kukamilisha kandarasi yake Arsenal licha ya kwamba klabu hiyo inataka kumuuza kutokana sababu za kifedhaHaki miliki ya pichaREUTERSImage caption

Lampard amtaka mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 22, kujiimarisha kufuatia usajili wa mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 24, kutoka RB Leipzig. (Metro)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, anasema kwamba anataka kushinda mataji zaidi akiichezea Chelsea na kwamba kuwasili kwa Warner kutampa changamoto zaidi . (Guardian)

Roy Hodgson anasema kwamba klabu ya Crystal Palace itafanya ujinga kupumzika na kujisahau na kufikiria hakuna timu itakayowasilisha ombi la kutaka kumnunua winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha mwisho wa msimu huu kutokana na athari za kifedha zilizosababishwa na Covid-19.. (London Evening Standard)

Roy Hodgson anasema kwamba klabu ya Crystal Palace itafanya ujinga kupumzika na kujisahau na kufikiria hakuna timu itakayowasilisha ombi la kutaka kumnunua winga wa Ivory Coast Wilfried ZahaHaki miliki ya picha

Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche anasisitiza Kwamba kiungo wa kati wa England Dwight McNeil, ambaye amehusishwa na Manchester United, Manchester City, Leicester na Juventus, hatouzwa kwa bei rahisi . klabu hiyo imedaiwa kuitisha dau la £50m ili kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sun)

Mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo, ambaye amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake anasema kwamba atakuwa na wakati wa kuzungumza kuhusu kandarasi mpya sasa baada ya ligi kurejea.. (Express and Star)

Mshambuliaji wa England Andy Carroll, 31, na beki wa Uhispania Javier Manquillo, 26, wanakaribia kutia saini kandarasi mpya na klabu ya Newcastle United. (Shields Gazzette)

Nuno Espirito Santo na mshambuliaji wa klabu hiyo TraoreHaki miliki ya pichan

Kiungo wa kati wa Ufaransa Papa Gueye, 21, amekubali kujiunga na Watford baada ya kandarasi yake katika klabu ya Le havre kukaribia kukamilika msimu huu , lakini wakala wake anasema kwamba hataki mchezaji huyo kujiunga na Watford na Arsenal tayari imempatia ofa huku nayo Marsaile ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zinamnyatia. (Le Phoceen, in French)

Steve Bruce anasema kwamba amechoka kusikiliza madai kwamba kazi yake ipo hatarini kama mkufunzi wa Newcastle iwapo uuzaji wa klabu hiyo utakamilika. Mkufunzi Mauricio Pochettino na Rafael Benitez wamehusishwa na klabu hiyo. (Telegraph)

Atletico Madrid ilikataa dau la $136m kumuuza mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 20, kutoka klabu ya Uingereza kabla ya mlipuko wa corona.. (Goal)

Atletico Madrid ilikataa dau la $136m kumuuza mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 20Haki miliki ya pichan


Post a Comment

0 Comments