BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 22-06-2020

Barcelona wameanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya wa mwaka mmoja kwa ajili ya Muargentina Lionel Messi, anayetimiza umri wa miaka 33 Jumatano wiki hii. (Marca)

Chelsea wanaweza kuelekeza nia zao kwa kiungo wa safu ya nyuma kushoto ya wa Paris St-Germain Layvin Kurzawa, 27, iwapo hawataweza kusaini mkataba na mchezaji wa Kimataifa wa England kutoka Leister Ben Chilell,23. (Express)

Juventus wako tayari kutoa ofa kwa mlinzi wa Italia Daniele Rugani, 25, na winga wa Italia Federico Bernardeschi, 26, kwa Wolves katika jaribio la kushusha gharama ya mkataba kwa ajili ya mshambuliaji kutoka Mexico Raul Jimenez, 29. (Tuttosport)

Kalidou KoulibalyHaki miliki ya pichaES

Liverpool wameweka dau la pauni milioni 54 kwa ajili ya mlinzi wa Napoli Msenegal Kalidou Koulibaly. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 pia anataka kuchezea timu za Manchester United na Chelsea. (Corriere dello Sport)

Roma wameipatia mlinzi wa Tottenham Mbelgiji Jan Vertonghen, 33, mkataba a miaka miwili unaomuwezesha kuchagua kuendelea kubakia huko kwa msimu wa tatu. (Il Messaggero, via Mail)

Mlinzi wa Tottenham Mbelgiji Jan Vertonghenmlinzi wa Tottenham Mbelgiji Jan VertonghenHaki miliki ya picha

Everton wamejiunga na mbio za kusaini mkataba na difenda wa Real Valladolid Mohammed Salisu, 21. Mchezaji huyo kutoka Ghana , ambaye alikua na kipengele cha thamani ya pauni milioni £10.8 cha kumuachilia katika mkataba wake, pia ana nia ya kuchezea Southampton na Manchester United. (Mail)

Kiungo wa kati wa Everton na Ufaransa Morgan Schneiderlin,30, amepanga kuondoka Goodison Park baada ya kufaulu katika viipimo vya afya vya Ligi ya Ufaransa. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Everton na Ufaransa Morgan Schneiderlin(kushoto) ana mpango wa kuondoka Goodison ParkHaki miliki ya picha

Klabu ya PFC Slavia Sofia inasema makubaliano yamefikiwa kwa ajili ya Manchester City kukamilisha kusaini mkataba na Mbulgaria anayecheza safu ya kati Filip Krastev, 18. (Manchester Evening News)

Afisa wa Birmingham City alinyenyuka katika kiti chake ili kumruhusu mama yake Jude Bellingham atazame mechi yao ya Championi katika West Brom. Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 16 Anasakwa na Manchester united na Borussia Dortmond

Post a Comment

0 Comments