BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMANNE TAREHE 16-06-2020


Leicester City wanapambana na Crystal Palace kuwania sahihi ya beki wa kati wa Burnley James Tarkowski, 27. (Mirror)

Manchester City wanamtazama kwa karibu beki wa kulia raia wa Morocco na mchezaji wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21. Kwa sasa anachezea kwa mkopo timu ya Borussia Dortmund (AS via Sun)

Juventus wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho, 28, na beki wa kushoto Muhispania Marcos Alonso,29. (Express)

Timo WernerHaki miliki ya picha

Uhamisho wa Timo Werner kutoka RP Leipzig kwenda Chelsea utakamilika rasmi juma hili, wakati mkataba wa mshambuliaji huyo wa Kijerumani wa pauni milioni 53 unakwisha leo. (Evening Standard)

Kiungo wa zamani wa Uholanzi Ronald de Boer amesema kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 23, angependa kuhamia Real Madrid kuliko Manchester United (Marca)

Nice itaweka dau la pauni milioni mbili kwa ajili ya kiungo wa kati wa Everton, Mfaransa Morgan Schneiderin, 30, juma hili (Mail)

Brentford and Algeria's Said BenrahmaHaki miliki ya picha

Chelsea imeanza mazungumzo ya kumnyakua winga wa Brentford Said Benrahma, 24. (RMC, via Express)

Nia hiyo ya Blues kwa Benrahma ni pigo kwa Aston Villa, ambao wamekuwa wakihusishwa na taarifa za kumtaka mshambuliaji huyo (Birmingham Live)

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho anataka kumsajili nahodha Thiago Silva, 35, anayekipiga Paris St-Germain kwa uhamisho huru msimu huu (Sun)

Ghana and Atletico Madrid's Thomas ParteyHaki miliki ya picha

Arsenal wanaripotiwa kuwa tayari kuongeza mshahara mara tatu wa kiungo wa kati Thomas Partey wa Atletico Madrid ili kumsajili mchezaji huyo wa Ghana, 27. (Goal,via Mirror)

Norwich wako karibu kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Sunderland Bali Mumba, 18. (Mail)

Post a Comment

0 Comments