BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 19-06-2020

Barcelona itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32, ya mkataba mpya ili kuendelea kuwa kwenye hiyo hadi 2023. . (Mundo Deportivo via Metro)

Mshambuliaji wa Uhispania Pedro, 32, amekubali kujiunga na Roma kwa uhamisho wa bila malipo na anatakiwa kuamua ikiwa atasaini mkataba wa muda mfupi kusalia Chelsea hadi mwisho wa msimu. (Guardian)

Hata hivyo, Pedro hayuko tayari kumaliza msimu na Blues kwasababu hataki kuhatarisha uhamisho wake wa Roma. (The Athletic - subscription only)

Aberdeen winger Ryan FraserHaki miliki ya pichaSNS

Kiungo wa kati wa Scotland Ryan Fraser, 26, anataka zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki kusaini mkataba wa kuwa wakala huria baada ya kukataa ofa ya mkataba wa muda mfupi kusalia Bournemouth kwa kipindi kilichosalia msimu huu. (The Times - subscription only)

Leicester City haitaki kumuuza beki wa kushoto wa Uingereza, 23, Ben Chilwell dirisha la usajili litakapofunguliwa - hata kama itapewa pauni milioni 50. (Sky Sports)

Bayern Munich itafikiria kumuuza beki wa kushoto wa Austrian David Alaba, 27, badala ya kukatiza mkataba wake. (Telegraph - subscription only)

Mikel ArtetaHaki miliki ya picha

Kocha Mikel Arteta ameitaka bodi ya Arsenal kumuunga mkono ili kuimarisha kikosi chake wakati wa kipindi cha usajili - baada ya mahasimu wao kwenye Ligi ya Primia Chelsea kukubali makubaliano ya pauni milioni 54 kumsaini mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 24, kutoka RB Leipzig. (Mirror)

Beki wa kulia wa Monaco na mchezaji Ujerumani pia Benjamin Henrichs, 23, ambaye anawindwa na Bayern Munich kuna uwezekano mkubwa akajiunga na RB Leipzig. (Bild Sport - in German)

Nahonda raia wa Ureno Nani, 33, anasema kwamba aliyekuwa mchezaji wa Manchester United ambaye pia ni wa kimataifa, Cristiano Ronaldo, 35, amesema kuwa bila shaka atajiunga na Ligi Kuu za soka kabla ya kustaafu. (ESPN)

Lincoln City boss Danny Cowley

Kocha wa Huddersfield Danny Cowley anaamini kwamba klabu hiyo iko vizuri wakati anapotafuta uwezekano wa kuongeza mkataba kwa walio kwenye mkopo akiwemo, mlinda lango wa Denmark Lossl, 31, na kiungo wa Uingereza Trevoh Chalobah, 20. (Yorkshire Post)

Mlinda lango wa Everton raia wa Ireland Dan Rose, 16, amehamia klabu ya Bundesliga club Schalke. (Liverpool Echo)

Post a Comment

0 Comments