BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS TAREHE 25-06-2020

Juventus imekubali dau la euro milioni 80 na Barcelona kumsaini mchezaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 Arthur - lakini bado watalazimika kumshawishi kiungo huyo kujiunga nao. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Portugal William Carvalho, 28, ameafikia makubaliano na klabu ya Leicester City , huku klabu hiyo ya Premia ikihitaji kukubaliana dau la uhamisho na klabu ya Real Betis. (Marca)

Crystal Palace inakaribia kumsaini Nathan Ferguson baada ya West Brom kuthibitisha kwamba beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 19 alikataa kutia saini kandarasi mpya. (Guardian)

Crystal Palace inakaribia kumsaini Nathan FergusonHaki miliki ya picha

Arsenal inatarajiwa kukubali kuongeza kandarasi ya beki wa Portugal Cedric Soares kwa mkopo kutoka Southampton na inataka kumsaini beki huyo kwa kandarasi ya kudumu baada ya uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Manchester United na England lder Dion McGhee, 19, ananyatiwa na West Ham, Rangers na AZ Alkmaar. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa England Andy Carroll, 31, anatarajiwa kutia saini kandarasi ya mwaka mmoja katika kandarasi yake iliopo na klabu Newcastle United . (Chronicle)

Andy CarrollHaki miliki ya picha

Wamiliki wa klabu ya West Ham hawako tayari kuiuza klabu hiyo baada ya ripoti kwamba kuna kampuni moja UAE inayovutiwa na klabu hiyo. (Star)

Mamlaka ya soka nchini England inatafuta njia ya kutumia kombe la Community Shield kama jaribio la kurudi kwa mashabiki kabla ya kuanza kwa msimu ujao. (Times - subscription required)

Gabriel MartinelliHaki miliki ya pichan

Kiungo wa kati wa Arsenal na Brazil Gabriel Martinelli, 19, huenda akakosa kushiriki katika mechi zilizosalia msimu huu baada ya kupata jeraha la goti wakati wa zoezi. (Mirror)

Kulikuwa na hatua kubwa zilizopigwa katika kupata uwanja mpya wa San Siro baada ya mkutano kati ya AC Milan na wakuu wa mji huo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Klabu ya Rennes imeipatia Monaco £13.55m) ili kumnunua beki wa Ufaransa Benoit Badiashile, 19. (RMC Sport - in French)

Post a Comment

0 Comments