BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AWATUMIA SALAMU ZA VITISHO WANAOTAKA KOMBE LA FA


Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesema baada ya kufanikisha lengo la kunyakua taji la Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2019/20 sasa wachezaji wako tayari kupambana kwenye michuano ya FA. Kikosi chetu kimejerea jijini Dar es Salaam leo mchana kutoka Mbeya na kuingia kambini moja kwa moja tayari kwa mchezo wa robo fainali ya FA dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho kutwa Jumatano Uwanja mkuu wa taifa Kocha Sven amesema katika mchezo wa jana alikuwa na malengo mawili ya kutafuta angalau pointi moja ya kuchukua ubingwa pamoja na kuhakikisha timu inakaa vizuri kabla ya kukutana na Azam. Sven amesema wachezaji wote wako fiti tayari kuipigania timu katika michuano ya FA ingawa amekiri mchezo dhidi ya Azam utakuwa mgumu. "Ilikuwa safari ndefu hadi kujihakikishia ubingwa kimahesabu haikuwa mechi rahisi, lengo letu ilikuwa tupate walau pointi moja na tumefanikiwa sasa tunahamishia malengo kwenye michuano ya FA. "Baada ya Ubingwa wa jana wote tuko vizuri na tayari kwa FA jana tumecheza kwa malengo mawili kupata pointi moja na kujilinda kwa ajili ya mechi ya Jumatano," amesema Kocha Sven.

Post a Comment

0 Comments