BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AFUNGUKA MIPANGO YAKE KUELEKEA UBINGWA LIGI KUU


Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesema baada ya ligi kusimama kwa takribani miezi mitatu wiki mbili hazikutosha kwa ajili ya kuandaa timu kabla ya kurejea ndiyo maana wanajitahidi kuwaweka sawa wachezaji kiakili, kimwili na kimbinu kila wakati. Kocha Sven amesema hakufurahia matokeo ya sare dhidi ya Ruvu Shooting siku ya Jumamosi lakini alifurahia jinsi wachezaji walivyokuwa wakitimiza majukumu yao uwanjani. Raia huyo wa Ubelgiji ameongeza kuwa wachezaji wote waliopata nafasi ya kucheza mechi dhidi ya Ruvu walionyesha hali ya kuhitaji kupata ushindi ingawa haukupatikana kama matarajio waliyokuwa wamejiwekea. "Ligi imesimama kwa miezi mitatu halafu tunajiandaa kwa wiki mbili lazima muda usitoshe. Tutaitumia hii wiki pia kuendelea kuwajenga wachezaji kimwili, kiakili na kimbinu kabla ya mchezo wetu ujao mwishoni mwa juma," amesema Kocha Sven. Sven pia amesema kama ikiwezekana wanaweza kupata mechi nyingine ya kirafiki kabla ya mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Mwadui FC ili kuwaweka wachezaji vizuri na kurudisha muunganiko wa timu. "Nafikiri tutacheza mechi nyingine ya kirafiki kabla ya mchezo wetu ujao wa ligi tunachohitaji wachezaji wetu wawe tayari kama ilivyokuwa kabla ya kusimama kwa ligi. "Nataka kila mchezaji apate dakika 70 au 90 ndiyo maana wachezaji ambao hawakucheza dhidi ya Ruvu niliwapanga kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Transit Camp asubuhi yake kwa hiyo kila mmoja amepata muda mwingi wa kucheza," amesema Sven.

Post a Comment

0 Comments