BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YATWAA UBINGWA WA 2019/20 KWA STAILI YA AINA YAKE


Klabu ya Simba imetangazwa rasmi kutwaa ligi kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2019/20 baada ya mchezo kumalizika bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons leo kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Huu unakuwa ni ubingwa wa tatu mfululizo ambapo klabu hiyo imeweka historia kwani imebakiwa na michezo sita mkononi kabla ya kumalizika kwa ligi. Sare ya leo imefanya Simba kufikisha alama 79 ambazo hakuna timu nyingine ambayo inaweza kuzifikisha katika hizo mechi sita zilizosalia. Katika mchezo huo haukuwa na ufundi sana huku timu zote zikicheza mipira mirefu kutokana na Uwanja wa Sokoine kutokuwa katika eneo la kuchezea. Timu zote zimeshambuliana kwa zamu ingawa milango ilikuwa migumu kutokana na uimara wa safu za ulinzi. Kikosi kinarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa maandalizi dhidi ya Azam FC katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya FA utakaopigwa Julai Mosi Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments