BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YABANWA MBAVU NA RUVU SHOOTING TAIFA


Klabu ya Simba SC imelazimishwa sare ya mabao 1-1dhidi  Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba walionekana kuingia uwanjani na dakika ya 12 tu walijiatia bao la kuongozwa lililofungwa na Shiza Ramadhani Kichuya. Dakika ya 37 Salum Mayanga aliisawazishia bao Ruvu shooting na kipindi cha kwanza kilimalizika kwa mabao 1-1.

Kipindi cha pili timu hizo ziliendelea kukamiana na mpaka dakika ya 90 zilitoshana kwa mabao 1-1.Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 72 kwenye michezo 29 iliyocheza na kuzidi kuusogelea ubingwa kwa tofauti ya pointi 18 dhidi ya Yanga na Azam.

Kikosi cha Simba SC kiliongozwa na ; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael/Mohamed Hussein ‘ dk68, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Muzamil Yassin, Hassan Dilunga/Deo Kanda dk68, Luis Miquissone/Miraji Athumani dk82, Medie Kagere, John Bocco na Shiza Kichuya/ Francis Kahata dk61.

Ruvu Shooting; Mohamed Makaka, Omary Kindamba, Kassim Simbaulanga, Rajab Zahir, Baraka Mtuwi, Zuberi Dabi, Abdulrahman Mussa/Said Dilunga dk79, Shaaban Msala, Graham Naftal/Moses Shaaban dk79, Fully Maganga/Sadat Mohamed dk70 na William Patrick/Jamal Mnyate dk63.

Post a Comment

0 Comments