Ligi kuu nchi nchini Ujerumani ilirejea mapema zaidi kwa ligi zinazocheza Michuano ya Ligi ya Mabingwa ulaya na kuifanya kukaribia kumalizika kabla ya juni 31 . Nimekuletea sababu zilizopelekea Bundesliga kurejea mapema zaidi
1.USHINDANI KATIKA LIGI
Ligi kuu
nchini Ujerumani ilikuwa ya kwanza kutangazwa kurejeshwa na chama cha soka nchini humo (DFL) .binafsi
naona ni jambo la busara kwa klabu hizo kukubali kumalizia msimu wao wa ligi bila utata .
Vilabu vimekubaliana kucheza mechi 9 kwa kila timu ili kumaliza
msimamo.Kutokana na ushindani mkubwa baina ya timu hizo ilikuwa ni ngumu kwa
DFL kutoa kombe kwa Bayern Munich anayeongoza kwa point 55 huku anayemfuata ni Borrusia
Dortmund akiwa na point 51,nafasi ya tatu ni RB. Leipzig wakiwa na point 50
huku M,glaidbach akiwa na point 49. Ni ngumu sana kwa msimamo kama huu kutoa
kombe kwa klabu yeyote .
Ukitazama
msimu wa 2018-19 ligi kuu Ujerumani imeonekana kuleta ushindani kuliko misimu
michache iliyopita . Bayern Munich alitwaa Bundesliga kwa tofauti ya point 2
dhidi ya hasimu wake B.Dortmund huku
akipishana kwa point 12 na aliye nafasi
ya tatu RB.Leipzg .
Ushindani
huu umeongeza ufuatiliwaji wa BundesLiga duniani kote baada ya kufanya vizuri
kwa vilabu vyake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya .
2. MAPATO NDANI YA BUNDESLIGA
Ligi ya
Ujerumani ni tofauti kabisa na ligi nyingine linapokuja suala la ukusanyaji
mapato. Wakati ligi mbali mbali zikijipatia faida kwa kuuza tiketi za mechi kwa
Bundesliga ni asilimia 14.1 tu ya mapato yanatokana na viingilio.
Bundesliga
inategemea zaidi Uuzaji na ununuzi wa wachezaji ambao huingiza asilimia 16.9 ya
mapato, Matangazo ya viwanjani asilimia 22.9
ya mapato huku asilimia 46.1 wakipata kupitia mikataba na vituo virushavyo
mechi hizo.
Mwaka 2008
BundesLiga ilikuwa na mapato ya Euro bilioni 1.7 huku mwaka 2019 ilikuwa na
mapato ya Euro bilioni 4.019 .
Na mwaka
2019 waliweka rekodi kwa kupata Euro Bilion 1.25 kupitia matangazo ya urushaji
wa televisheni
Kwa takwimu
hizo unaweza kusema BundesLiga inaweza kuchezwa bila mashabiki na ikapata faida
pasipo hasara.
0 Comments