BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID YAZIDI KUKOMAA KWENYE MSIMAMO WA LIGI


Klabu ya Real Madrid imezidi kuikomalia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Hispania La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mallorca. Madrid walipata bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa kijana Vinicius Junior dakika ya 19 huku Sergio Ramos akikandamiza bao la pili dakika ya 56 kwenye mchezo huo.

Matokeo hayo yanaifanya Madrid kufikisha pointi 68 sawa na Barcelona na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi hiiyo zikiwa zimebaki mechi saba tu kwa ligi hiyo kumalizika.

Kikosi cha Real Madrid kilianza na : T.Courtious,Carvajal,Ramos,Varane,Mendy,Valverde,Modric/Toni Kroos, Bale/Asensio,Hazard/Diaz,Junior/Isco, Benzema/Mariano. 

Post a Comment

0 Comments