BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID WAREJEA KILELENI MWA LA LIGA

Klabu ya Real Madrid merejea kileleni mwa ligi kuu nchini Hispania La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhdi ya Real Sociedad. Sergio Ramos alikuwa wa kwanza kuipa Real Madrid bao la kuongoza kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 50 huku Karim Benzema akifunga bao la pili dakika ya 70. Sociedad hawakuwa nyuma kwani walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 83 lililofungwa na Mikel Merino . 

Matokeo hayo yanaifanya Real Madrid kuongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 65 sawa na Barcelona huku wakizidiwa tofauti ya mabao mawili lakini wanakaa nafasi ya kwanza kwa sheria ya Hispania kwamba ukishinda mchezo dhidi ya mpinzani wako na mkalingana pointi basi atakaa juu yako hata kama umemzidi magoli ya kushinda.

Post a Comment

0 Comments