BETI NASI UTAJIRIKE

NIYONZIMA ATANGAZA BALAA ZITO KWA WATAAKAOCHEZA NA YANGA


Kiungo mshambuliaji wa Yanga Haruna Niyonzima amefunguka mipango waliyonayo kuelekea kukamilisha mechi nane zilizobaki za ligi kuu Tanzania . Kupitia mahojiano maalumu Niyonzima amekiri kuwa mwaka huu hawana nafasi ya kutwaa Ubingwa na malengo yao ni kumaliza nafasi ya 2 . Niyonzima amenukuliwa akisema 

"Tuna mechi ngumu kwenye ligi hilo lipo wazi kwani kwa sasa timu nyingi zinapambana hasa ukizingatia ni lala salama, nasi tuna mipango yetu ya kutoacha kushinda kwenye mechi ambazo tutacheza.
“Kitu cha msingi ni kuona tunakusanya pointi tatu ambazo zitatufanya tuzidi kuwa kwenye nafasi nzuri, hatutaki kumaliza tukiwa nafasi ya tatu tunahitaji ya pili,
Hii leo klabu ya Yanga itakwaana vikali na klabu ya Namungo FC yenye washambuliaji wakali Lusajo na Bigirima katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam

Post a Comment

0 Comments