Waziri wa Habari ,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe ameendelea kukazia suala la usajili wa wachezaji wa kigeni . Mwakyembe ametaka vilabu vipunguze idadi ya wachezaji kutoka 10 mpaka watano .
Mbali na hilo ameweka mkazo kwa matajiri wanaotaka kumiliki hisa nyingi ndani ya vilabu vya Simba na Yanga na amewapa ushauri wa kuanzisha timu zao. Mwakyembe ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha Redio cha EFM jijini Dar es salaam na hapa ninamnukuu
"Nilitoa muongozo Klabu zote zilizoanzishwa na wananchi ziendelee kuwa mali ya wananchi na kama kuna wawekezaji basi wamiliki 49%. Kama wawekezaji wana misuli basi watengeneze timu zao"
"Iwapo tathmini ya kweli ikifanyika kufahamu thamani za timu kama Yanga Sc na Simba SC timu hizo haziwezi kuwa na thamani ya bilioni 20 tu kama za Simba"
"Natoa changamoto kwa vilabu vyote hakikisheni mnafanya tathmini za vilabu vyetu. Binafsi naona zina thamani ya zaidi ya matrilioni na sio bilioni kama wanavyosema"
"Sisi kama serikali lazima tutoe vibali vya kufanya kazi suala la wachezaji sijui 10 wa kigeni me binafsi sikubaliani nalo, TFF hili wanalifanyiaje kazi"
"Hatuzuii wachezaji wa kigeni, ila kama timu ipo ligi kuu inatakiwa ichukue wachezaji wanaotoka ligi kuu nchi husika. hatuwezi chukua chukua tu watu hovyo hovyo"
0 Comments