BETI NASI UTAJIRIKE

NAVY KENZO WAGEUKIA RASMI SOKA LA VIJANA , NAHREEL AFUNGUKA MIPANGO YAO


Producer na Msanii wa kizazi kipya Emanuel Mkono maarufu kwa jina LA Nahreel na msanii mwenza Haika  wamegeukia rasmi soka la vijana. wanamuziki hao wanaoeunda kundi la Navy Kenzo wamedhamilia kukuza soka la vijana kwa kuanzisha timu za vijana chini ya miaka 15 na chini ya miaka 17.

NavyKenzo linakuwa kundi la kwanza la wasanii wa bongo fleva kumiliki timu ya soka wakiwa na malengo ya kuwasaidia vijana kufikia ndoto zao hususani soka . NavyKenzo wanatamba na ngoma ya Why Now wamekuwa wakisaidia kukuza vipaji vijana kuanzia muziki na sasa soka .

Kundi la Navy Kenzo  linamiliki timu ziitwazo NavyKenzo U15,NavyKenzo U17 na Champions. Akihojiwa na mwandisho wetu Nahreel amesema 

"Lengo letu ni kukuza soka la vijana hivyo tumeanzia huku kwa vijana wadogo kabisa na kupitia hawa naamini tutaibua vipaji vya kutosha kwa timu ya taifa hapo baadaye".

Champions U17 na NavyKenzo U17 zimeingia fainali na mchezo huo utapigwa hii leo mchana wa saa 2:00 kwenye uwanja wa Tanganyika Packers kawe jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments