BETI NASI UTAJIRIKE

MOTO WA SIMBA HAUZIMIKI,WAWEKA REKODI MPYA NDANI YA UWANJA WAO WA MAZOEZI MO ARENA


Klabu ya Simba imezidi kuwapa raha mashabiki wa soka nchini baada ya hapo jana kucheza michezo miwili ya kirafiki na kupata ushindi  kwenye michezo hiyo. Mchezo wa kwanza ni ule dhidi ya Transit Camp na wapili ni dhidi ya KMC.

Mechi hizi mbili zilipigwa kwa nyakati tofauti ndani ya Mo Simba Arena na zilikuwa nikivutio kikubwa kwa mashabiki wliofika uwanjani hapo kutazama michezo hiyo

Simba vs Transit Camp

Mchezo huu ulichezw majira ya asubuhi na kikosi kiliongozwa na  Aishi Manula, Haruna Shamte Gadiel Michael Kennedy Juma, Pascal Wawa ,Jonas Mkude ,Hassan Dilunga, Said Ndemla, John Bocco,Luis Miquissone, Shiza Kichuya

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kushind kwa mabao  4-2 wafungaji wakiwa Kanda ,Tairone,Fraga na Kagere

Simba vs KMC 

Mchezo huu ulichezwa majira ya jioni na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Magoli ya Simba yalifungwa na John Bocco akifunga mawili pamoja na Ibrahim Ajibu.

Simba inakuwa klabu ya kwanza kwa mwaka 2020 kucheza mechi mbili ndani ya siku moja ikitumia uwanja wake wa mazoezi 

Post a Comment

0 Comments