BETI NASI UTAJIRIKE

MORISSON KWISHA HABARI YAKE ,MWAKALEBELA AMPA ZA USO


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa Yanga ina mambo mengi ya kuyazungumza kuliko kumzungumzia mchezaji wao Bernard Morrison.

Kumekuwa na mvutano kati ya Morrison na uongozi wa Yanga kuhusu ishu ya mkataba wake ambapo yeye Morrison anasema kuwa dili lake linameguka msimu ukiisha huku Yanga ikisema kuwa bado ina mkataba naye wa miaka miwili.

Mwakalebela amefunguka kuwa, wanahitaji kufanya usajili ulio makini na wa kiwango cha juu msimu ujao ili kuepuka changamoto za hapa na pale kutoka kwa wachezaji na timu kuwa chini ya kiwango.

“Kwa sasa mtazamo wetu haupo kwa Morrison, kuna mambo mengi ya kufanya na ya kuyazungumzia katika klabu yetu ya Yanga kuliko kumzungumzia yeye.

“Tunajipanga kuhakikisha tunakuwa makini zaidi katika usajili wa msimu ujao wa ligi kuu, tunahitaji kuwa na kikosi kipana kilicho imara na cha ubingwa, kila mchezaji atakayepata nafasi ya kusajiliwa ni lazima awe anapata nafasi katika timu aliyotokea.

“Kwa sasa tunajipanga kuhakikisha tunafanikiwa kushinda mechi zote zilizo mbele yetu na ule mchezo wa FA ili kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani.”

Post a Comment

0 Comments