BETI NASI UTAJIRIKE

MKUDE KUREJEA DIMBANI DHIDI YA MWADUI

 

Kiungo mkabaji Jonas Mkude chaguo namba moja la Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck ameaanza mazoezi mepesi akiwa chini ya jopo la madaktrai wa timu hiyo linaloongozwa na Yassin Gembe.

Mkude anauguza maumivu ya vidole viwili aliyopata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC uliochezwa Juni 8,2020 Uwanja wa Mo Simba Arena.

Mkude anaendelea na mazoezi mepesi ambayo yatamfanya arejee kwenye ubora wake aliokuwa nao kabla ya kuumia akiwa chini ya uangalizi maalum.

Tayari ameukosa mchezo wa Juni 14 uliopigwa Uwanja wa Taifa atakosa pia mchezo wa Juni 20 utakaopigwa Taifa dhidi ya Mwadui FC.

Mkude kibindoni amehusika kwenye jumla ya mabao manne ambapo amefunga mawili na kutoa pasi mbili za mabao kati ya 64 ya Simba.

Post a Comment

0 Comments