BETI NASI UTAJIRIKE

MBWANA SAMATTA HALI YAZIDI KUWA MBAYA ARSENAL WAKICHEZEA KICHAPO

Ligi kuu Uingereza (EPL) imerejea hapo jana kwa michezo miwili tangu kusimama wake mwezi machi kwa janga la Corona. Mchezo wa kwanza ni ule wa Aston Villa vs Shiffield United uliomalizika kwa sare ya 0-0 na kuwafanya Aston Villa kusalia nafasi ya 19 wakiwa na pointi 26. Mbalii na Samatta kuingia kipindi cha pili lakini alishindwa kuisaidia timu hiyo kupata ushindi.


Mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Arsenal vs Manchester City.mchezo huu ulimalizika kwa Arsenal kupigwa mabao 3-0 huku David Luiz akipata kadi nyekundu dakika ya 49 .
Rahim Sterling alikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 45 huku Kelvin De Bruyne akifunga bao la pili kwa mkwaju wa Penati dakika ya 51 huku Super sub Phil Foden akitokea benchi alifunga bao la 3 dakika ya 88.Arsenal alielemewa kwenye mchezo huo baada ya kupiga mashuti matatu tu ambayo hayakulenga hata lango huku Manchester city wakipiga mashuti 17 na 11 yakilenga golini. Manchester City waliutawala mchezo kwa Asilimia 6 dhidi ya 35 za Arsenal.
Matokeo hayo yanaifanya Manchester City kufikisha pointi 60 ikicheza michezo 29 na kubaki nafasi ya pili huku Arsenal akibaki nafasi ya 9 akiwa napointi 40 baada ya michezo 29.

Post a Comment

0 Comments