BETI NASI UTAJIRIKE

MBAO FC WAENDELEA KUTOA KIPIGO KWA POLISI TANZANIAMbao FC  wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya wapinzani wake Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezawa Uwanja wa CCM Kirumba.Wazir Junior mshambuliaji namba moja ndani ya Mbao FC alijaza kimiani bao hilo dakika ya 65 lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.

Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini imeyusha pointi tatu mazima leo mbele ya Mbao FC.

Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Mbao inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro ambaye alianza kushinda mbele ya Coastal Union bao 1-0.Licha ya ushindi huo Mbao inabaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 32 na kujikusanyia pointi 29.

Post a Comment

0 Comments