BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER CITY YAENDELEZA VICHAPO KUELEKEA UBINGWA EPLKlabu ya Manchester City imeendelea na kampeni za kuwinda ubingwa wa ligi kuu Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Burnley. Mchezo huo ulipigwa dimba la Etihad na Manchester City kuonyesha umahili mkubwa. Mshambuliaji anayechipukia Phil Foden alikuwa wa kwanza kuifungia manchester City bao la kuongoza dakika ya 22 na 63 huku Riyad Mahrez akifunga bao dakika ya 43 na 45+3 . Bao jingine lilifungwa na David Silva dakika ya 51 .

Safu ya Ushambuliaji ya Manchester City imekuwa hatari kwani imefunga mabao 76 huku safu ya ulinzi ikiwa dhaifu kwa kuruhusu mabao 31 kwenye mechi 30 walizocheza. Mshambuliaji Kun Aguero anaongoza kwa mabao ndani ya timu hiyo kwa kufunga mabao 16.

Matokeo hayo yanawafanya Manchester City kufikisha pointi 63 wakicheza michezo 30 hivyo kuongeza presha kwa Liverpool wanaohitaji pointi 5 tu waweze kutangazwa mabingwa wapya wa Primia Ligi.

Post a Comment

0 Comments