BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA AKERWA NA KAULI ZA MASAU BWIRE BAADA YA SARE NA RUVU SHOOTING


Msemaji wa klabu ya Simba Haji S.Manara ameonekana kukerwa na kauli za msemaji wa klabu ya Ruvu shooting Masau Bwire baada ya kutoka sare ya mabao 1-1. Manara katika mtandao wake wa kijamii amepost video ya msemaji huyo akihojiwa na wanahabari baada ya mechi masau bwire  alinukuliwa akisema 

"Ni kudra za mwenyezi Mungu tu ambazo zimewafanya Simba wapate sare maana haya matokeo kwa upande wetu hayakuwa mazuri.Ujue kuna watu kutoka nje ya nchi wamenipigia simu kunipongeza namna ambavyo tumecheza soka na wakisema sisi tunastahili pengine kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ,Simba wana bahati sana 

Naye manara aliandika 

Ngoja leo nimpaishe huyu Mwalimu, tatizo hata sijui kama anatumia insta 🤪
but kiukweli Ruvu wamecheza vzuri na walionyesha miili yao ipo tayari.. Ila ni vema wachezaji wetu wakaona hii clip, wakasikia ngebe za Mwalimu Bwire, wakaelewa vema pain tunayokumbana nayo huku site, kama ilivyo desturi ya klabu za Tanzania zikipata sare tu na cc sherehe mwaka mzima.

Najua mlitaka kushinda lakini mshabiki hataki neno kutaka, kwake yy ni ushindi tu, na hao ndio mabosi zetu wanaoifanya Simba iwe kubwa.
Go Go Go VS Mwadui, No Excuse Wanaume

Post a Comment

0 Comments