BETI NASI UTAJIRIKE

LA LIGA WATOA RATIBA RASMI YA MECHI ZITAKAZOPIGWA KUANZIA ALHAMISI HII



Ligi kuu nchini Hispania maarufu kam La Liga inarejea tena baada ya kusimama kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na janga la Corona . Ligi hiyo itanza kuchezwa siku ya alhamisi tarehe 11 kwa mchezo kati ya Seville vs Real Betis mchezo utakaopigwa saa tano usiku.

Kurejea kwa La Liga ni shangwe kwa mashabiki wa Real Madrid na Barcelona timu ambazo zina ushindani mkali kueleke kutwaa kombe la ligi hiyo. Barcelona amecheza michezo 27 akiwa na pointi 58 huku Real Madrid akiwa na pointi 56 baada ya michezo 27.

Kwa upande wa mbio za ufungaji bora nyota wa Barcelona bado anaongoza kwa kufunga mabao 19 akifuatiwa na Karim Benzema mwenye mabao 14. 

Mechi hizo zitapigwa bila ya mashabiki kuwepo uwanjani na zinategemewa kutazamwa dunia nzima . 

Ratiba ya mechi za La Liga 



Post a Comment

0 Comments