BETI NASI UTAJIRIKE

KWELI DAVID MOLINGA BABA LAO AWANUSURU YANGA NA KIPIGO


Mashabiki wa Yanga wamekoshwa na kiwango cha mshambuliaji wa klabu hiyo David Molinga baada ya kuwanusru na kuichapo kutoka kwa Namungo FC.Yanga wakiwa     Nyumbani jijini Dar es salaa wameponea chupuchupu kuchapwa baada ya kulazimisha sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kwa sare hiyo, Yanga SC inafikisha pointi 57 ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja na Azam FC inayoshika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 78 baada ya wote kucheza mechi 31.

Yanga wanapaswa kumshukuru mshambuliaji wao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga Ndama ‘Falcao’ aliyetokea benchi na kufunga mabao mawili dakika 10 za mwisho kuinusuru timu yake kuadhirika nyumbani.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliochezeshwa na refa Hussein Athumani wa Mwanza, aliyesaidiwa na Rashid Zongo wa Katavi na Athumani Rajab wa Iringa zilimalizika bila mabao.
Na dakika saba tu baada ya kuanza cha pili, Namungo walipata bao la kwanza lililofungwa na beki wa zamani wa Yanga SC, Edward Charles Manyama aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Jukumu Kibanda kabla ya kufunga la pili dakika ya 70.

Molinga ambaye siku za karibuni amekuwa akizomewa na mashabiki wa timu hiyo akaifungia Yanga dakika ya 80 bao la kwanza na la pili dakika ya 90 akimalizia kazi nzuri ya mtokea benchi mwenzake, kiungo Abdulaziz Makame.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul, Adeyoum Ahmed, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Feisal Salum, Balama Mapinduzi/Tariq Sief dk58, Haruna Niyonzima, Patrick Sibomana/David Molinga dk58, Ditram Nchimbi/Raphael Daud dk72 na Deus Kaseke/Abdulaziz Makame dk84.
Namungo FC; Nourdne Balora, Miza Kristom/Rogers Gabriel dk89, Jukumu Kibanda/Edward Charles Manyama dk46, Stephen Duah, Carlos Protas, Daniel Joram/Hamis Fakhi dk46, Hashim Manyanya, Lucas Kikoti, Bigirimana Blaise, Reliants Lusajo na George Makang'a/Jamal Issa dk82.

Post a Comment

0 Comments