BETI NASI UTAJIRIKE

KUREJEA KWA EYMAEL LEO MCHANA KWAIBUA SHANGWE JANGWANI
Habari njema kwa  wanayanga kwani koch mkuu wa klabu hiyo Luc Eymael anawasili leo mchana akitokea kwao nchini Ubelgiji. Kocha huyo anarejea rasmi siku tatu kabla ya mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga na Mwadui.

Kocha huyo amenukuliwa akisema Nilipanga kurudi Juni 7 ila kuna mambo hayakukamilika kwa upande wa usafiri, kwa sasa ninatarajia kurejea rasmi Juni 10 kuendelea na majukumu yangu," amesema

Eymael anarejea siku chache baada ya kulalamikia uongozi wa klabu hiyo kushindwa kumtumia tiketi ya ndege tangu mapema ili kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria walioingia kambini tarehe 27 mei mwaka huu.

Mashabiki wamefurahishwa na kurejea kwa Eymael kutokana na timu hiyo kushindwa kuonyesha uwezo mkubwa kwa mechi za kirafiki iliyochezwa ukiwemo mchezo dhidi ya  KMC ambao Yanga  walipigwa mabao 3-0

Post a Comment

0 Comments