BETI NASI UTAJIRIKE

KISA MORRISON YANGA YASHTAKIWA SIMBA TFF


Uongozi wa klabu ya Yanga rasmi umepeleka malalamiko Shirikisho la soka nchini (TFF) kuhusu kushawishiwa winga wake Bernard Morrison kujiunga na klabu nyingine kinyume Cha sheria,ili haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu katibu Mkuu wa Yanga Wakili Simon Patrick amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na Winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea.

"Mchezaji wetu ameeleza kila kitu,hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kutolea maamuzi."

Patrick amesema tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Post a Comment

0 Comments