BETI NASI UTAJIRIKE

KAGERE AFUNGUKA USIYOYAJUA KUHUSU KAPTENI JOHN BOCCO


Kinara wa mabao, Medie Kagere amemchambua Nahodha John Bocco kuwa ni kiongozi imara ambaye siku zote anaamini katika ushindi. Kagere ambaye anacheza sambamba na Bocco katika idara ya ushambuliaji amesema nahodha huyo siku zote mhamasishaji mkuu wa kupata alama tatu uwanjani. Raia huyo wa Rwanda, amesema Bocco ni mtu mpole, imara na anajua anachokifanya na amekuwa akimkubali ndani na nje ya uwanja. "Bocco ni mtu safi, mpole na kiongozi imara na anatuongoza katika njia nzuri na wakati wote anatuhamasisha katika kutafuta ushindi uwanjani. "Siku zote anaamini katika ushindi na ikitokea tumepoteza au kutoka sare utamuona anakosa amani na anakuja kwetu na kutupa moyo tusahau yaliyopita," amesema Kagere. Kagere anaongoza katika kufumania nyavu kwenye VPL ambapo hadi sasa ametupia mabao 19 huku mechi zikiwa zimebaki tisa kabla ya ligi kumalizika.

Post a Comment

0 Comments