BETI NASI UTAJIRIKE

HAALAND AMFANYA TIMO WERNER AONEKANE SI KITU

Mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Erling Halaand amemfanya Timo Werner asionekane kitu kwenye mchezo wa Bundesliga.Mchezo huo wa Rb Leipzig dhidi ya Borrusia Dortmund ulipigwa dimba la Red Bull arena na ilikuwa ni kipimo kwa nyota hao wawili

.Haaland alionekana Bora zaidi kwa kufunga mabao mawili dakika ya 30 na 90 na kuifanya Dortmund kuondoka na point 3 muhimu zilizowafanya kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Timo Werner amekwishamalizana na Chelsea na kinachosubiriwa kwa sasa ni yeye kuelekea Stamford bridge kwa msimu wa 2020/21. Timo Werner amekuwa na kiwango kizuri msimu huu baada ya kufunga mabao 26 Bundesliga nyuma ya Lewandowski mwenye mabao 33.

Post a Comment

0 Comments