BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL: MORRISON HAENDI KOKOTE KWA SASA


Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amefunguka  hatma ya winga wa kikosi hicho, Mghana, Bernard Morrison, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba.

Ikumbukwe kuwa, tangu Machi, mwaka huu kulikuwa na taarifa zilizokuwa zikimhusisha Morrison kujiunga na Simba, wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii, Morrison alisikika akidai kuwa alipewa dola 5000 (milioni 11, 560, 000), ikiwa kama sehemu ya kumshawishi atue Simba.

Eymael amesema Morrison hawezi kwenda Simba kwa sababu tayari ameshasaini Yanga na kama ikitokea akasaini Simba basi atafungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kwa muda wa miaka miwili.

Unajua Morrison tayari ameshasaini Yanga, hawezi tena kwenda Simba, kama ikitokea akasaini Simba, basi ni lazima atafungiwa na FIFA, kwa muda wa miaka miwili kama ambavyo sheria inasema,” amesema Eymael.

Morrison amecheza mechi 10 za ligi na kuhusika kwenye mabao sita kati ya 32 yaliyofungwa na yanga, akifunga matatu na kutoa pasi tatu.

Post a Comment

0 Comments