BETI NASI UTAJIRIKE

EYMAEL ATAKIWA KUREJESHWA NCHINI KUINUSURU YANGA BAADA YA KIPIGO CHA 3-0KMC imeiadhibu klabu ya Yanga kwa kipigo cha mabao 3-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa dimba la Uhuru jijini Dar es salaam. Lengo la mchezo huo ni kujipima uwezo kabla ligi kuu haijarejea tarehe 13 juni .

Sadala Lipangile alikuwa wa kwanza kuipatia KMC bao la kuongoza dakika ya 31 ya mchezo huo huku Charles Ilanfya akifunga bao la pili dakika 45 na bao la tatu ilifungwa na Hasan Kabunda.

Mchezo huo uliibua maswali kwa baadhi ya wachezaji na mashabiki uwanjani hapo na kulalama wakimtaka mkufunzi mkuu Luc Eymael arejeshwe nchini kuendelea kukinoa kikosi hicho chenye maskani yake Kariakoo Jangwani.


Post a Comment

0 Comments