Kocha mkuu wa Yanga hajafurahishwa na kitendo Cha Morrison kutoshiriki na wenzake kuikabili Mwadui Fc Mchezo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dimba la kambarage mkoani shinyanga.
Eymael amenukuliwa akisisitiza mchezaji huyo kuwaomba radhi wachezaji wenzake kwa kitendo hicho
"Mimi sikuwepo, nimekutana na mambo mengi ambayo si ya kawaida ndani ya klabu, kama kocha mkuu ni jukumu langu kutatua na kuiweka sawa timu.
"Niliongea na Morrison na kunieleza tatizo lake hadi kunizimia simu. Kuna baadhi ya mawakala wa soka wana matatizo na wanarubuni wachezaji, hata hivyo hilo ni kosa lake na anatakiwa kuomba radhi.
"Najua kuwa Morrison kwa sasa ndiye mchezaji nyota wa Yanga, hilo halina ubishi, lakini lazima ajue umaarufu wake unatokana na msaada au ushirikiano na wenzake, hilo ni jambo muhimu kujua, Yanga ni timu na wala si ya mchezaji mmoja pekee."
0 Comments