BETI NASI UTAJIRIKE

ERASTO NYONI AFUNGUKA SARE NA MWADUI,ATOA AAHIDI HII


Kiraka Erasto Nyoni amewaomba wapenzi na mashabiki wa Simba SC, kusahau matokeo ya sare dhidi ya Ruvu Shooting yaliyopatikana wiki iliyopita badala yake waendelee kuisapoti timu katika mechi zinazofuata kama ilivyokuwa kabla. Erasto amesema kwa upande wao kama wachezaji wameshasahau kuhusu matokeo hayo na tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya Mwadui FC. Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi kwa ufanisi mkubwa amewataka mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani na wasivunjike moyo kwa matokeo yaliyopita kwani ana imani furaha yao itarudi muda si mrefu. "Sisi tumeshasahau kuhusu matokeo ya mchezo uliopita, tunajipanga kwa ajili ya mechi inayofuata. Mashabiki wetu tunaomba muendelee kutuunga mkono wala msivunjike moyo kwa kilichotokea. "Wachezaji wote tuko kwenye hali nzuri morali yetu ipo juu na tunashukuru hatuna majeruhi tunachotaka ni kuhakikisha tunarejesha furaha kwa mashabiki wetu ambao mara zote wamekuwa upande wetu," amesema Erasto. Erasto ni mmoja wa mihimili ya kikosi cha Simba katika idara ya ulinzi sambamba na Pascal Wawa, Kennedy Juma, Tairone Do Santos na Yusuph Mlipili.

Post a Comment

0 Comments