BETI NASI UTAJIRIKE

DONALD NGOMA NA AZAM WAMALIZANA RASMI

Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam raia wa Zimbabwe Donald Ngoma ametupiwa virago na Klabu yake hiyo.

 Ngoma alijiunga na Azam FC akitokea Yanga SC mkataba wake umememalizika na aliyekuwa anahitajika kutoa tamko juu ya kuendelea kuwepo ndani ya kikosi hicho alikuwa ni Kocha Mkuu, Aristica Cioaba ambaye kwa sasa amesharejea.

Habari zinaeleza kuwa pande zote zimekubaliana kwa mchezaji huyo kusepa mazima ndani ya Azam FC bila kumuongezea dili jingine.

Msimu uliopita Ngoma alikuwa ni namba moja kwa utupiaji ambapo alitupia mabao 10 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Msimu huu wa 2019/20 Ngoma ametupia mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao.

Post a Comment

0 Comments