BETI NASI UTAJIRIKE

AKINA SAMATTA WAPIGWA TENA NA WOLVES


Mbwana Ally Samatta leo amecheza kwa dakika zote timu yake, Aston Villa ikichapwa 1-0 na Wolverhampton Wanderers FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.

Aston Villa ambao leo wamecheza mechi ya nne ndani ya siku 11, sasa wamefikisha mechi nane za ligi bila kushinda na mbaya zaidi wanaonekana wana tatizo kubwa katika safu yao ya ushambuliaji.


Kipigo hicho kinazidi kuwachimbia kaburi Aston Villa, wakibaki nafasi ya 19 na pointi zao 27 baada ya kucheza mechi 32. 
Aston Villa wapo juu ya Norwich City inayoshika mkia kwa pointi zake 21 za mechi 31 na nyuma West Ham United na AFC Bournemouth zenye pointi 27 pia za mechi 31 ambao kwa pamoja wanaifuatia Watford yenye pointi 28 za mechi 31.
Tayari Lverpool wamejihakikishia taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya waliokuwa wapinzani wao kwenye mbio hizo, Manchester City kuchapwa 2-1 na Chelsea juzi.

Liverpool imetwaa ubingwa kwa rekodi ikiwa imebakiza mechi saba baada ya kufikisha pointi 86 katika mechi 31, ikifuatiwa kwa mbali na Man City yenye pointi 63, Leicester City pointi 55 na Chelsea pointi 54 wote wakiwa wamecheza mechi 31.


Wolverhampton baada ya ushindi wa leo inafikisha pointi 52 kufuatia kucheza mechi 32 wakipanda nafasi ya tano mbele ya Manchester United inayobaki na pointi zake 49 mbele ya Tottenham Hotspur 


Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Nyland, Konsa/Elmohamady dk60, Hause, Mings, Targett/Taylor dk10, Nakamba/Trezeguet dk82, Douglas Luiz, Hourihane/McGinn dk60, Grealish, Davis/El Ghazi dk82 na Samatta.


Wolves: Rui Patricio, Boly, Coady, Saiss, Doherty, Dendoncker, Neves, Joao Moutinho, Jonny, Jimenez/Neto dk84 na Jota/Traore dk60

Post a Comment

0 Comments