BETI NASI UTAJIRIKE

VAN GAAL HAKUSTAHILI KUONDOKA MAPEMA MANCHESTER UNITED


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney anaamini kocha Luis Van Gaal hakustahili kuondoka klabuni hapo mara baada ya kudumu Old Trafford kwa misimu miwili na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.

Luis Van Gaal alijiunga na Manchester United akichukua nafasi ya David Moyes msimu wa 2014-15 na msimu huo alimaliza nafasi ya 4 huku msimu wa 2015-16 akitwaa FA dhidi ya Crystal Palace lakini akimaliza nafasi ya 5. Tangu kufukuzwa kwa Van Gaal Manchester United imeingia top four mara moja tu msimu wa 2017/18 na kuifanya ionekane timu dhaifu tangu kuondoka kwa Ferguson.

Wayne Rooney amenukuliwa akisema "Nilijiskia furaha kufanya kazi na Van Gaal ila nilihisi kuharibiwa alipoondolewa . Tulitakiwa tumuache kwa msimu wa tatu naamini tungeimalika "

"Mambo yalianza kubadilika na wachezaji walielewa falsafa yake na ndani ya miaka miwili nilijifunza mengi zaidi kuliko makocha wengine wote na ndio maana namshukuru sana si kwa sababu alinifanya kapteni bali kwa jinsi alivyokuwa ananiamini 

Rooney aliondoka Manchester United mwaka 2017 na kujiunga na klabu yake ya utotoni Everton

Hizi hapa takwimu za makocha walioifundisha Manchester United tangu Alex Ferguson aondoke klabuni hapo

Post a Comment

0 Comments