BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE TAREHE 26-05-2020

Everton imewasilisha ombi la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29, lakini klabu hiyo inataka dau la £60m kumuuza raia huyo wa Brazil. (Il Mattino - in Italian)
The Toffees pia wamewasilisha ombi la $25m kwa Barcelona kumnunua beki wa Ufaransa Jean -Claire Todibo ,20, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Schalke nchini Ujerumani. (Mail)
Manchester United kumuongezea kandarasi kipa wa England Dean HendersonHaki miliki ya pichan
Manchester United itamuongezea kandarasi kipa wa England Dean Henderson, 23 ili kumruhusi kumaliza msimu wake na klabu ya Sheffield United huku kandarasi yake ikitarajiwa kukamilika mwezi Juni. (Telegraph)
Mmiliki wa Bournemouth Maxim Demin karibu aiuze klabu hiyo kwa mfanyabiashara wa Saudia mnamo mwezi Januari , kabla ya makubaliano hayo kugonga mwamba kuhusiana na thamani ya klabu hiyo. (90min)
Phillipe Coutinho
Kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich huenda asicheze tena baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kuamua kutomsaini kwa mktaba wa kudumu kutoka Barcelona, na sasa ananyatiwa na Chelsea, Arsenal na Tottenham. (Sky Sports)
Chelsea imeamua kutotumia kifungu chake cha sheria dhidi ya winga wa Ivory Coast Jeremie Boga ,20, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda kuichezea klabu ya Napoli. (Guardian)
Mauro IcardiHaki miliki ya pichan
Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 27, anakaribia kuhamia katika klabu ya Paris St-Germain kwa dau la £54m. (ESPN)
Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa£34m. (Todofichajes)

Post a Comment

0 Comments