BETI NASI UTAJIRIKE

MAAGIZO YA RAISI MAGUFULI YAIBUA SHANGWE SIMBA ,UBINGWA WANUKIARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli amesema kasi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini imeendelea kupungua ambapo amesema hali ikiendelea kuwa hivyo anaweza kuruhusu vyuo vikafunguliwa wiki ijayo pamoja na kuruhusu shughuli za Michezo

Akizungumza mapema leo Mjini Chato, Rais Magufuli alisema idadi ya wagonjwa wa corona katika vituo mbalimbali imepungua sana huku kasi ya maambukizi nayo ikiendelea kupungua

"Hali ya maambukizi imepungua sana. Amana ilikuwa na wagonjwa 198 wamebaki 12 tu. Mloganzila 30 wamebaki 6. Kibaha 50 wamebaki 22. Arusha kituo cha Moshono kina wagonjwa 11 vingine havina wagonjwa. Mwanza vituo 10 wagonjwa 6. Dodoma wagonjwa 42 wamebaki wawili tu"

"Kama hali itaendelea hivi hadi wiki ijayo nimepanga kufungua vyuo ili wanafunzi wetu waendelee kusoma. Pia nimepanga kuruhusu michezo kwa sababu michezo ni sehemu ya burudani, Maisha lazima yaendelee," alisema Rais Magufuli

Sasa ni wazi mshike-mshike wa ligi kuu ya Vodacom unaweza kurejea mapema tu pengine kabla ya Juni. Shangwe zimeibuka kwa  mashabiki wa Simba kwani wamebakiza mechi 5 tu kukabidhiwa kombe hilo.

Post a Comment

0 Comments