BETI NASI UTAJIRIKE

MICHAEL JORDAN AUZA VIATU VYA MTUMBA KWA BILIONI 1.29

Jozi za viatu za nguli wa mchezo wa kikapu Michael Jordan za mwaka 1985 zimeweka rekodi ya kuuzwa kwa kiasi cha dola za Marekani 560,000 sawa na Tsh 1,295,504,000 mnada wa mtandaoni.
Jozi hiyo ya viatu ya Nike Air Jordan 1s, ilivaliwa na Jordan wakati wa msimu wake wa kwanza akiwa kinda na klabu ya Chicago Bulls. Awali ilitarajiwa vigeuzwa kwa dau la kati ya dola 100,00 mpaka dola 150,000 kwenye kampuni ya mauzo ya Sotheby's.
Rekodi ya zamani ilikuwa dola za Marekani 437,500 kwa jozi ya viatu vya Nike 'Moon shoes' vya mwaka 1972.
Jordan alivaa jozi ya viatu vya namba mbili tofauti, mguu wa kushoto namba 13 na mguu wa kulia namba 13.5.
Air Jordan 1s ziliuzwa na Jordan Geller, aliyeanzisha jumba la kumbukumbu la mkufunzi Shoezeum huko Las Vegas.
Uuzaji huo uliambatana na makala ya Netflix ya 'The last dance'na picha za nyuma ya pazia za wakati Bulls walipokuwa wakisaka taji la sita la NBA msimu wa 1997-98.
Jordan anapigiwa chapuo kuwa ndiye mchezaji bora zaidi wa kikapu kuwahi kutokea, hivyo kwa viatu vyake vya msimu wa kwanza kuuzwa kwa bei hiyo si jambo la kushtukiza sana japo halikutarajiwa awali.
Jordan trainersHaki miliki ya pichaImage

Post a Comment

0 Comments