BETI NASI UTAJIRIKE

MEDDIE KAGERE ATHIBITISHWA KUREJEA MAPEMA BONGO


Mshambuliaji namba moja ndani ya Simba Meddie Kagere anatajwa  kuwa miongoni mwa nyota ambao watarejea mapema kuungana na wachezaji waliobaki Bongo kuanza mazoezi.

Kagere aliibukia Rwanda baada ya mapumziko ya lazima yaliyotokana na Janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.

Habari zinaeleza kuwa tayari jitihada zimeanza kufanyika kumrejesha nyota huyo ili aendelee pale alipoishia kwenye ligi akiwa ni kinara wa utupiaji.

"Kagere ni miongoni mwa nyota ambao wanaweza kurejea mapema kwani uongozi unatambua mchango wake hiyo ataungana na wachezaji wenzake mapema," ilieleza taarifa hiyo.

Kagere ndani ya ligi ni kinara wa kutupia mabao ambapo amefunga mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao huku Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao 63.

Post a Comment

0 Comments