BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA: WAFAHAMU WAFUNGAJI 5 BORA BUNDESLIGA TANGU KUANZISHWA KWAKE
Kwa wanaofuatilia BundesLiga nadhani hawawezi kushtushwa na orodha ya wafungaji bora wa muda wote BundesLiga. Ligi hii ilianzishwa mwaka 1963 na imekuwa na washambuliaji makini walioweka historia kubwa kwenye soka. Hawa hapa ni wafungaji  10 bora muda wote kwa BundesLiga 

1.Gerd Muller-Magoli 365

Gerd  Muller ndiye baba wa ujerumani kwenye suala la ufungaji ,Rekodi yake imekuwa ni ngumu mno kufutika tangu alipoanza soka mwaka 1965-1979 akiichezea Bayern Munich na alifanikiwa kutwaa mataji manne ya ligi hiyo. Alitwaa kiatu mara 7 na mara 5 kati ya hizo alifunga mabao mengi zaidi ya mechi alizocheza .msimu wa mwaka 1971/72 alifunga mabao 40 na rekodi hiyo haijavunjwa mpaka leo

2. Klaus Fischer-Magoli 268

Fischer alicheza michezo 100 zaidi ya Gerd Muller lakini alichwa nyum kwa mabao 97. Fischer alifunga mabao 182 akiitumikia schalke 04 lakini pia aliichezea 1860 Munich,Cologne na Buchum. Mshambuliaji huyu alidumu Bundesliga kutok mwaka 1968-1988 n kumfanya awe na miaka 20 kwenye ligi hiyo3. Robert Lewandowski-Magoli 227

Lewandowski ndiye mchezaji pekee wa karne ya 21 aliyeingia kwenye orodha hii . alianza na Borrusia Dortmund aiitumikia kwa misimu minne na kufunga maba0 74 kisha alihamia Bayern Munich alikofunga mabao 153 mpaka sasa. Mbali na kwamba anamiaka 31 lakini anauwezo mkubwa wa kufunga na mpaka sasa anaongoza mbio za ufungaji mabao akiwa na mabao 27 msimu wa 2019/204.Jupp Henkey- Magoli 220

Henkey anafahamika kama kocha mwenye mafanikio makubwa BundesLiga lakini pia ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye ligi hiyo.Henkey amezichezea Borrusia Monchenglash na Hannover kwa miaka 14 na kutwaa kombe la ujerumani mara 4 huku pia akiwa mfungaji bora wa muda wote kwa klabu ya Borrusia Monchenglash akiwa na mabao 195 


5. Manfred Burgsmüller -Magoli  213 

Toka mwaka 1967 mpaka 1990 Manfred fundi wa kupiga chenga alijizolea umaarudu na kupewa jina la utani "Manni". huyu ni mchezaji aliyechezea vilabu vigi zaidi kama Essen,Dortmund ,Nurnberg na Bremen. Manni ndiye mfungaji bora muda wote kwa klabu ya Dortmund akifunga mabao 135 . Mara baada ya kustaafu soka alihamia marekani na kuchezea America Football Team kama mfungaji na mwaka 2019 mei alifariki akiwa na miaka 69.


Post a Comment

0 Comments