BETI NASI UTAJIRIKE

BORRUSIA DORTMUND VS BAYERN MUNICH HAPO KESHO JE UPO UPANDE GANI SHABIKI WA SIMBA NA YANGA




Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa soka naamini utakuwa ukiisubiri kwa hamu mechi ya mahasimu wawili wa Ujerumani .Nazungumzia Bayern Munich Vs Borrusia Dortmund maarufu kwa jina la kijerumani Der Klassiker  kiingereza wanaita The Classic na Kihispanyola wanaita German Classico.

Hapo kesho mahasimu hawa watakutana nyumbani kwa Dortmund dimba la Signal Iduna Park majira ya 7:30 usiku na mchezo huu utapigwa bila mashabiki   

Mchezo wa kwanza ulimalizika kwa Bayern Munich kushinda mabao 4-0 dhidi ya Dortmund. mara ya mwisho Dortmud kuifunga Bayern Munich ni mwaka 2018-Novemba 10 wakishinda kwa 3-2  huku ikipewa vipigo viwili vikubwa kile cha tarehe 6 april 2019 walifungwa 5-0 na kile cha 31 machi 2018 walifungwa 6-0 

Mechi hii inategemewa kutazamwa na watu zaidi ya milioni 100 kupitia Runinga na hapa tanzania itaonyeshwa kupitia Star Times 

Robert Lewandowski na Haaland wanategemewa kufanya makubwa kutokana na kuonyesha uwezo wa hali ya juu na lolote linaweza kutokea kwenye mechi hiyo.

Mechi nyingine zitakazopigwa hapo kesho na jumatano ni hizi zifuatazo

Post a Comment

0 Comments