BETI NASI UTAJIRIKE

BUNDESLIGA YAWEKA HISTORIA MPYA KWA MWAKA 2020



Ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga imerejea kwa kishindo baada ya Lock Down ya miezi miliwili iliyosababishwa na COVID-19. BundesLiga imerejea na kuweka historia mpya kwa mwaka 2020 . Ligi hiyo imerejea mapema zaidi na imegeuka kivutio kwa mechi tisa zilizochezwa hapo wikiendi.

Takwimu kutoka skysports wenye haki ya kuonyesha mechi za ligi hiyo nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza mechi za jumamosi zilitazamwa na watu milioni 6 na uwanjani kulikuwa na wachezaji na viongozi pekee.

Sky wanasema watazamaji milioni 3.68 walilipia kutazama mechi hizo huku watazamaji milioni 2.45 wakitazama bure kupitia mtandao wa Konferenz. Hii ni mara ya kwanza kwa ligi hiyo kutazamwa na watu wengi kwa siku moja ndani ya Ujerumani huku mechi ya Borrusia Dortmund dhidi ya Schalke 04 ikiwa kivutio zaidi kutazamwa huku Dortmund wakishinda mabao 4-0.

Zaidi ya terevisheni 70 zilirusha live michezo hiyo ya BundesLiga na kunauwezekano watazamaji zaidi ya milioni 100 walitazama mechi hizo duniani kote.

Post a Comment

0 Comments