BETI NASI UTAJIRIKE

NUGAZ AZUNGUMZIA UJIO WA MAKAMBOWakati mashabiki na wanachama wa Yanga wakiwa na kiu ya kuona mshambuliaji wao kipenzi, Mkongomani Heritier Makambo akirejeshwa klabuni hapo, uongozi wa klabu hiyo umesema katika usajili ujao lolote linaweza kutokea na wapo katika mchakato wa kumrejesha straika huyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema wapo katika mikakati mikubwa ya kumrejesha mshambuliaji huyo pamoja na wachezaji wengi ambao wamependekezwa na Kocha Mkuu, Mbelgiji Luc Eymael.

Alisema Kamati ya Utendaji ya Yanga na ile ya usajili kwa kupitia nguvu kubwa ya wadhamini wao, GSM na SportPesa hakuna linaloshindikana na kwamba suala la dola laki tatu kwa klabu hiyo si tatizo linapokuja suala la kumpata mchezaji anayehitajika na benchi la ufundi

"Kurejea kwa Makambo lolote linaweza kutokea kwani tayari mchakato unaendelea kwa mchezaji huyo na wengine watakuwa kuijenga Yanga na kurejea heshima yake, dola laki tatu si tatizo kwa Yanga," Nugaz amenukuliwa 

Nugaz amesema mipango ya kamati ya Utendaji ni kufanya usajili kabambe ili msimu ujao timu iwe ya ushindani mkubwa na kuwapa raha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Mbali na Makambo, tayari uongozi wa Yanga umepanga kukaa meza mmoja na Azam FC kwa ajili ya mazungumzo kumnasa kiungo Salum Abobakar 'Sure Boy'.'

Makambo aliondoka Yanga msimu uliopita baada ya kuuzwa na kusaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Horoya FC ya Guinea

Post a Comment

0 Comments