BETI NASI UTAJIRIKE

UONGOZI MTIBWA WATOA MAAGIZO KWA WACHEZAJI NA MASHABIKIOfisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kuwa watanzania na mashabiki wanapaswa wachukue tahadhari ya Virusi vya Corona kwani ni janga la dunia nzima.

Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Serikali ilizuia mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara.

Mtibwa Sugar ilivunja kambi yao Machi 17 na sasa wachezaji wapo nyumbani wakiendelea na mazoezi binafsi ambayo wamepewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kifaru amesema: :-"Tumewaambia wachezaji wetu wawe makini na kujilinda na Virusi vya Corona pia tunapenda kuwaomba mashabiki na watanzania kiujumla kuchukua tahadhari kujilinda na Virusi vya Corona,".

Post a Comment

0 Comments